Loading ...

0
UjuziNet . 12th Jun, 2021

Usipojifunza kuuza, Utauzwa au Utauziwa

Tufanye kuna watu wawili. Mtu wa kwanza ana wazo kubwa sana linaloweza kuibadili dunia. Labda wazo hilo linaweza kuwa sawa na Facebook au Uber ya sasa.Nikukumbushe kuwa yapo mawazo makubwa zaidi ya facebook au uber, na kuna watanzania nimekutana nao wenye mawazo makubwa mpaka unatetemeka lakini hawajui kuuza.

 

Mtu wa pili yeye hana wazo la kutisha kiivyo. Kwa kifupi ni kuwa hana wazo kabisa lakini mtu huyu yupo busy kujifunza sanaa ya kuuza kila siku. Akiamka asubuhi yeye ni kujifunza sanaa ya kuuza tu. Kuuza kuuza kuuza…..

 

Wakati mtu wa kwanza yeye anaamka na kuja na mawazo makubwa makubwa kama mtume aliyeoteshwa.

 

Huyu mtu wa pili yeye anakesha usiku na mchana kujifunza sanaa ya kuuza.

 

Nikiwa mwekezaji kamwe sintaweka pesa zangu kwa mtu wa kwanza mwenye mawazo makubwa makubwa. Nitawekeza pesa zangu kwa mtu anayekesha usiku na mchana kujifunza sanaa ya kuuza.

 

Kwa mfano, wa Ray Croc na hawa wakaka wawili Dick na Mac McDonald waliokuja na wazo la McDonalds ungewekeza kwa nani?

 

Ngoja nikupe mifano ya watu maarufu unaowajua DUNIANI.

 

 

Mtu wa kwanza ni Mark Zukerberg unamjua? Najua unamjua….na utasema

 

yeye ndiye aliyekuja na wazo kubwaaa la Facebook. SI KWELI. Huu utafiti utakushtua kidogo. Nifuatilie. Nitakuelezea. Facebook ilianza Desemba 2004. Unajua nani alianzisha wazo la facebook? Wote tunamjua Mark Zuckeberg si ndiyo?

 

Sasa leo ninakuambia ukweli aliyebuni wazo kubwa la facebook ni Mapacha wawili waliojulikana na kama Winklevoss brothers. Walikuwa na wazo kubwaa la facebook lakini Mark Zuckerberg akalichukua. Au Unaweza kusema aliiba, aliwapora, vyovyote vile utakavyosema lakini yeye ndiye aliyesimamisha Facebook ikafahamika hivi leo.

 

Mark Zuckerberg akiwa ni mwanafunzi aliitwa na hawa wakaka Winklevoss Brothers wakiwa wote ni wanafunzi kutoa mawazo yake kuhusu mfumo kama wa facebook ambao tayari walikuwa wameshautengeneza kwa hatua za awali lakini haukuwa hewani . Walitaka mawazo yake kwasababu Mark alikuwa


 

mzuri sana kwenye coding yaani kutengeneza mfumo. Akausoma mfumo wote kwa umakini halafu kesho yake akaanza kuutengeneza mfumo wao kama ulivyo. Akamshirikisha rafiki yake Eduardo aweke hela ili mfumo uwekwe hewani.

 

,   Eduardo alitoa $18,000 mfumo ukaingia hewani. Mwanzo ilijulikana kama The

 

Facebook na ilikuwa kama Harvard‟s yearbook. Fuatilia movie moja muhimu kuhusu facebook iitwayo, The Social Network utanielewa.

 

Mfumo ulipowekwa hewani , hawa vijana akina winklevoss brothers walishtuka kwasababu wazo lao lilichukuliwa mchana kweupe, walienda kushtaki kwa mkuu wa chuo lakini walichemka.

 

Zuckerberg hakuishia hapo, alijua kabisa lile wazo linamhitaji mtu mmoja muhimu sana kuliko kawaida ambaye ni muuzaji. Bahati nzuri muuzaji tayari alikuwa ameshafuatilia kuhusu facebook ambaye ilikuwa inasambaa pale chuoni na kutumika na wanafunzi karibu wote. Jina lake ni Sean Parker. Kama humjui Sean Parker, huyu ndiye mwanzilishi wa Napster. Huyu jamaa ni muuzaji/sales guy. Mimi hupendelea kuwaita watu kama hawa wauza maono.

 

Unaweza ukawa na maono yako, wakayaona kisha wanahakikisha dunia nzima imeyajua maono hayo, wakaleta hela, wakaleta wawekezaji wakaleta wateja… Ogopa sana uwe na wazo kubwa halafu ukutane na muuza maono..umeliwa. Unamkumbuka Ray Croc?

 

 

Zuckerberg akamwambia Parker nina wazo kubwa sana linaloweza kutuingia mamilioni ya dollas. Parker akasema hapana hili siyo wazo la mamilioni, hili ni wazo la mabilioni ya dolla.

 

Parker akaungana na Zuckerberg …wakaingia kupiga kelele. Parker akafanikiwa kuuza maono ya facebook kwa mwekezaji mmoja jina lake ni Peter Thiel, akawekeza dola 500,000 mpaka facebook ilipofika level ilipo leo.

 

Dunia nzima ikaijua Facebook ni kitu gani kwasababu iliingia katika mikono ya muuzaji, Sean Parker.

 

Leo hii Zuckerberg ana thamani ya $56 billion, wakati Sean Parker, muuzaji ana thamani ya $2.6 billion. Haya sasa hawa akina Winklevoss brothers waliokuja na wazo kubwa la facebook wanamiliki nini?

 

Winklevoss brothers waliishia kumpeleka Mark polisi kwa bahati ndipo walipofanikiwa kupata fidia ndogo ambayo ni ya thamani ya $200 million tu wakati wenzao ambao si waanzilishi wa hilo wazo wanamiliki mabilioni.


 

Wasingekuwa na hela kabisa, kama mahakama isingeamua walipwe hicho kiasi.

 

Hivi wewe unadhani kama Mark Zuckeberg asingelichukua wazo hilo, kungekuwa facebook leo?

 

Kama Sean Parker muuzaji , asingeingia tungekuwa na Facebook?

 

Mfano mwingine ni Martin Eberhard, unamjua huyu mtu? Hebu google uone. Huyu ndiye aliyekuja na wazo la Tesla. Ndiyo mwanzilishi wa Tesla, lakini dunia nzima inamfahamu tajiri mkubwa duniani Elon Musk, mimi huyu jamaa namuita mwanamapinduzi akawa kama mwanzilishi wa Tesla. Elon Musk hakuanzisha Tesla, alipogundua kuwa Tesla inaweza kuwa mapinduzi makubwa kiuchumi duniani, akachukua hatua. Akanunua, akaingia sokoni na kuuza visheni ya Tesla. Leo hii ana zaidi ya $20 billion wakati mwenye wazo hajulikani na hana utajiri wowote.

 

Kama huuzi, utauzwa na hata wazo lako kubwa ulilonalo linabebwa. Sina maana wewe uibe mawazo ya watu na kuuza maono hayo duniani. Pointi yangu ni kwamba, ukubwa wa wazo si chochote kama hutaamua kuwa kama akina Ray Croc,Mark Zuckeberg, Sean Parker, Elon Musk na wengine wengi. Kama hutaamua kuwa muuzaji sahau mafanikio. Hata kama mawazo ni makubwa vipi. Jifunze kuuza. Jifunze kuuza jifunze kuuza. Tutazama zaidi kuhusu kanuni kuu saba za kuuza.

 

Kuna wazalishaji wengi sana lakini kuna uhaba wa watu wanaoweza kuuza mawazo. Ukijifunza kuuza, kila mtu atakuhitaji. Acha tabia ya kutafuta mawazo makubwa zaidi ya Apple, snapchat au facebook, jenga msingi wako kwenye sanaa ya kuuza maono. Ukijifunza kuuza hutakosa hela hata kama huna wazo kubwa.



Jisajili kusoma kozi ya KUONGEZA MAUZO


Shopping Cart

Loading...