ANZA. Hapa ni pale ambapo unaingia rasmi kwenye biashara, baada ya kuhakiki wazo lako kwa wateja wachache sasa unaingia kwa kuwafuata wateja wengine wengi kulingana na kianzio chako. Hapa ni muhimu sana ukumbuke, wazo lililo kichwani halina maana kama hujachukua hatua yoyote. Ili uweze kubuni na kuja na wazo zuri la biashara lazima ujiulize watu wanapata usumbufu gani ?Unawezaje kuondoa usumbufu huo au kurahisisha maisha yao au kupunguza gharama au kuokoa muda wao au kutatua matatizo yao kama magonjwa au maumivu?
Mfano, umewahi kujiuliza kwanini watu wanapendelea kutumia UBER na siyo Taxi za kawaida?
Ule usumbufu wa mimi kutembea mpaka barabarani kutafuta Taxi za kawaida, Usumbufu wa kumsubiri dereva wa Taxi muda mrefu barabarani na anaweza asifike na asijali kabisa.
Natumia UBER kwasababu inanipunguzia muda wa kusubiri, kuniondolea usumbufu na kunirahisishia.
Soma sekta unayotaka, fuatilia muda unaotumika mpaka mteja kupata huduma au bidhaa, fuatilia usumbufu anaokumbana nao halafu angalia namna ya kuja na njia rahisi ya kuondoa usumbufu na kumrahisishia.
Tuanze na hivi, Chagua sekta unayotaka halafu fuata hatua zifuatazo:
- MOJA,Soma mfumo mzima wa huduma wa sekta hiyo.
Soma mfumo mzima wa kununua bidhaa mbalimbali za matumizi ya kawaida.
Soma mfumo mzima wa kununua au kumiliki nyumba.
Soma mfumo mzima wa kupata huduma za hospitali na hata kuonana na daktari.
Soma mfumo mzima wa kuandaa chakula
Soma mfumo mzima wa kujenga nyumba mpaka kuhamia
Soma mfumo mzima wa kupata mke au mume wa maisha yako.
Soma mfumo mzima wa kilimo mpaka bidhaa inamfikia mteja.
Soma mfumo mzima wa kupata nyumba ya kupanga au ofisi
2. MBILI, orodhesha hatua au stepu zote za mfumo wa huduma.
Yaani hapa namaanisha, orodhesha hatua zote ambazo mteja lazima azipitie ili aweze kupata huduma au bidhaa anayotaka. Zipo hatua ngapi?
Kwa mfano, nikitaka kununua bidhaa za wakulima kwa jumla nitapitia hatua ngapi mpaka nipate bidhaa hizo? Lazima niende sokoni asubuhi na mapema kuanzia saa 11 asubuhi au kabla ya hapo. Nitakutana na madalali wa sokoni wenye maneno mengi. Ikishindikana hapo, lazima nisafiri vijijini kwa wakulima, muda mwingine lazima nitafute sehemu ya kulala, lazima nione bidhaa zipo kwenye ubora mwenyewe, lazima nimlipe mkulima atakayeniuzia mazao hayo, lazima nitafute usafiri wa kusafirisha mazao yangu na hatua nyingine nyingi ambazo sijataja. Yaani ni usumbufu na kero za kutosha. Sekta nyingi Afrika zipo hivyo.
3. TATU; Njoo na njia ya kupunguza hatua au stepu za mfumo wa huduma.
Baada ya kujua mfumo mzima na hatua ambazo mteja lazima azipitie ili aweze kuhudumiwa, njoo na ubunifu au njia ya kupunguza baadhi ya hatua hizo. Hii ipo hata kwenye taasisi kubwa kubwa kama hospitali na mashule au hata taasisi za Serikali. Unajua nini, kampuni ikiwa kubwa huwa inakuwa na mambo mengi, sheria nyingi zinazohitaji kujaza sehemu nyingi. Inachukua muda mrefu na hatua nyingi sana mpaka mteja kupata huduma au bidhaa. Vipi je kama ukija na majibu ya kupunguza hatua zinazopoteza muda? Wateja wangapi watafurahia huduma yako?
Sekta karibu zote zinahitaji mapinduzi haya. Utagundua kwamba zina hatua nyingi sana mpaka mteja apate huduma au bidhaa ambazo hazina maana na ni usumbufu kwa wateja. Je unaweza kuja na majibu ya kupunguza hatua hizo na kuhudumia wateja kwa urahisi?
4. NNE, Fanya majaribio kwa wateja wachache waone namna ambavyo umepunguza hatua zisizo na umuhimu na onyesha namna ambavyo umerahisisha na kuondoa usumbufu.
5. TANO, baada ya majaribio kwa wateja wachache, angalia wapi unaweza kuboresha au kurekebisha.
6. SITA, ingia sokoni na kuanza kuuza huduma au bidhaa zako ambazo zimetokana na wewe kupunguza mlolongo wa hatua zisizo za lazima. Umerahisisha na kuondoa kero Fulani.
Sikiliza nikuambie ndugu yangu, sekta zote zina kero ambazo zinatokana na mlolongo wa hatua ambazo mteja lazima azipitie zisizo za lazima. Zinapoteza muda, zinagharimu maisha ya watu, zinakera na ni usumbufu kwa mteja, Ukija na majibu ya kupunguza hatua hizo, tayari umeondoa kero Fulani au usumbufu Fulani.
Katika Sehemu ya Tatu , nitakupa mifano ya taasisi mbalimbali au biashara mbalimbali ambazo zimepitia hatua hizo kutatua kero, au usumbufu Fulani.
INGIA KATIKA KOZI HII BUREEE LAKINI KWA MUDA FULANI. WALE WATAKAOFANIKIWA KUJISAJILI MWANZONI NA KUANZA KUSOMA NDIYO WATAKAOFAIDIA NA KUENDELEA KUSOMA KOZI HII BUREE . SIKU ZIJAZO KOZI HII ITAWEKWA BEI NA ITAUZWA KWA WALE WATAKAOCHELEWA KUJIUNGA NA KUJISAJILI NDANI YA UJUZINET.
Ninao uhakika kwamba wabunifu wengi watazaliwa baada ya kujua hatua mbalimbali kwa mifano na kuondoa kero au usumbufu katika sekta Fulani.
Jisajili na kuanza kusoma kozi hii buree
Jisajili kwa kozi nyingine nyingi ndani ya UjuziNet na ambazo zinaingizwa na kuongezwa kila siku.